Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lowassa aahidi kuchunguza upya Sakata la Operesheni Tokomeza



Mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa Awamu ya Tano, ataunda tume tatu ikiwamo ya kuchunguza upya sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili ambalo utekelezaji wake ulilalamikiwa na wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda mkoani hapa, Lowassa alitaja tume nyingine kuwa ni za kuchunguza mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa la Efatha na wananchi na mgogoro kati ya wakulima.

“Kuhusu Operesheni Tokomeza wananchi wengi wamekuwa wakija kuniona na kunieleza wazi kuwa licha ya madhara yaliyojitokeza katika operesheni hiyo hawakulipwa, pia walipoteza haki zao, ndugu na mifugo."

Lowassa aliyetokea Namanyere alikofanya mkutano mwingine wa kampeni, aliwataka wananchi kuichagua Ukawa, kwa maelezo kuwa umoja huo utaleta mabadiliko.

Operesheni Tokomeza Ujangili ilibuniwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kupambana na ujangili ambao ulikithiri hadi taasisi za kimataifa kuingilia kati.

Hata hivyo, ilisitishwa Novemba Mosi, 2013 ili kupisha uchunguzi wa malalamiko yaliyojitokeza, yakiwamo ya wananchi kuuawa, kuteswa na kuporwa mali zao. 
 
Uchunguzi huo ulifanywa na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na sakata hilo lilipowasilishwa bungeni na kamati hiyo, lilisababisha mawaziri wanne kushinikizwa na Bunge kujiuzulu, kutokana na kuhusishwa na yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo.

Mawaziri waliong’oka ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Hamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Dk Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi).

Hata hivyo, hivi karibuni Ikulu iliwaondolea doa mawaziri hao kutokana na ripoti ya Tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo kwa maelezo kuwa waliwajibika kisiasa na hawakuhusika moja kwa moja na vitendo hivyo na hakuna hatua inayostahili kuchukuliwa dhidi yao.
 
 Kuhusu mgogoro wa kanisa la Efatha na wananchi alisema: “Suala hili linalalamikiwa sana na kwa muda mrefu linawatesa wakulima na wawekezaji. Katika kuwalinda wakulima wadogowadogo itaundwa tume ili kuchunguza suala hili ili hatua za haraka zichukuliwe.”

“Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi kati ya wakulima na wafugaji, hasa waliopo katika Bonde la Mto Rukwa. Nitaunda tume ili kuhakikisha kuwa naondoa migogoro hii ambayo imedumu kwa muda mrefu,” alisema.

“Serikali yangu itanunua mahindi kwa wakulima na itawalipa riba. Haya ndiyo mabadiliko ninayoyataka. Wanaosema hawana sera wanajidanganya sana nawaambieni mkinipa kura nikaingia Ikulu wataisoma namba,” alisema.

Mbowe: Tumeunganisha nguvu
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Tumeunganisha nguvu za Watanzania wenye dhamira na mapenzi mema wanaotaka kuona mabadiliko ya nchi yetu. Tumempokea Lowassa kwa sababu tunaamini atatusaidia safari yetu ya kuwakomboa Watanzania.

“ Mgombea (Lowassa) ameteswa sana CCM na ndoto yake ya uongozi ilikuwa siku nyingi, lakini CCM hawakuiona hiyo na wakampuuza kwa maneno ya uongo.”

Mbowe alisema Rais Kikwete alimtosa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa urais na kushangazwa na kitendo cha Pinda kuendelea kubaki CCM.

Mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Lowassa nao walichukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM, lakini baada ya kutopitishwa kuwania urais walihamia Ukawa.

Kada mpya wa Chadema, Hamis Mgeja alisema: “Miradi ambayo Magufuli (Dk John) alishindwa kuijenga kwa ubora itajengwa na kumalizwa chini ya utawala wa Lowassa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top