Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akikabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Jesha Salim Jecha huko hoteli ya Bwawani
mjini Zanzibar
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Jesha Salim Jecha akionesha fomu
za kugombea Urais wa Zanzibar, baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, huko hoteli ya
Bwawani mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo
amerejesha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC).
Maalim
Seif amerejesha fomu hizo majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za
tume hiyo zilizoko Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, baada ya
kukamilisha masharti yaliyowekwa na Tume hiyo.
Miongoni
mwa masharti hayo ni pamoja na kula kiapo mahakamani pamoja
kuambatanisha shilingi milioni mbili, mambo ambayo ametayatekeleza.
Baada
ya kukabidhi fomu hizo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Jecha Salim
Jecha, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
ameitaka tume hizo kufanya kazi kwa uhuru na uadilifu.
Amesema
kufanya hivyo kutapelekea kufanyika kwa uchaguzi wa amani, huru na wa
haki, jambo ambalo litailetea sifa kubwa Zanzibar katika jamii ya
kimataifa.
Katika
hafla hiyo, Maalim Seif ameambatana na baadhi ya viongozi wa Chama
hicho wakiwemo Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Malindi Mhe. Ismail Jussa
Ladhu, Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Chukwani Mhe. Mansoor Yussuf
Himid na Mratibu wa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Rashid.
Post a Comment