Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MPIGIENI KURA MAGUFURI-MAMA SALMA KIKWETE



 Na Magreth Kinabo –Maelezo,Lindi
MKE wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini  kuhakikisha kwamba wanapiga kura ya ndiyo kwa mgombea wa kiti cha urais,Dkt. John Magufuli , mgombea kiti cha Ubunge Hassan Kaunje na wagombea viti cha udiwani  ili waweze kupata maendeleo.
 
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Mama   Kikwete ,ambaye  pia  ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya     Taifa ya  Chama Cha Mapinduzi(NEC) wa Wilaya Lindi ,wakati wa uzinduzi  wa kampeni ya chama hicho ya wilaya hiyo ili  iliyoambatana na uzinduzi wa Ilani ya CCM kwa lengo la kuinadi  na kuwanadi wagombea hao iliyofanyika kwenye uwanja wa Fisi.
 
“Leo nimekuja kufanya kazi hii moja  ya kuhakikisha mgombea wa kiti cha urais,  anashinda akiwemo  mgombea wa kiti cha ubunge na wagombea  wa viti  vya  udiwani,” alisema Mama Kikwete huku akiinadi picha ya mgombea wa kiti cha urais  na kumnadi mgombea wa kiti cha Ubunge  na wagombea viti vya  udiwani katika kata mbalimbali kupitia chama hicho.
 
 Mama Kikwete  aliongeza kwamba  ikiwa kila mtu atatoka na kufanya kampeni ya nguvu jimbo hilo litapata kura ya ndiyo viti hivyo. 
 
Alisema  wananchi hao endapo  watafanya hivyo ifikapo Oktoba 25, mwaka huu, watakuwa wamefanya kazi iliyokamilika na watapata maendeleo kwani amani inapatikana  mahali ambapo kuna maendeleo. 
 
Pia aliwataka wananchi hao kuhakikisha watunza kadi zao za kupigia kura, wasije wakapoteza nafasi hiyo muhimu. 
 
Mama Kikwete aliwataka wananchi hao, kukipa chama hicho kura ya ndiyo kwa sababu kina ilani, ni chama makini  na kinafanya kazi kwa mipango.
Akizungumzia kuhusu ilani ya chama hicho,Mama Kikwete alisema,ina mambo makubwa manne, ambayo ni kuondoa umasikini, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, kuendeleza vita ya kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Katika uzinduzi huo, Mama Kikwete alimkabidhi  vitendea kazi mgombea wa kiti cha Ubunge  ,ambavyo  ni Katiba ya CCM na ilani hiyo ili  aweze kufanya kazi  huku akishangiliwa na mamia ya watu walijitokeza uwanjani hapo wengi wao wakiwa ni vijana.
 
Pia aliwapokea wanachama wapya  12 kutoka Chama Cha Wananchi(CUF) walioongozwa na Laibu Kais, ambaye alikabidhi kadi na bendera ya chama hicho  na kuahidi kupeperusha bendera ya CCM  kila kata.
 
Kaisi na  waliokuwa wagombea wenzake wa kiti cha Ubunge 10 wameungana ili kumwuunga mkono Kaunje, hatua ambayo ilipongenzwa na Mama Kikwete.
 
“ Kura zipotosha huwezi kuhama kwenda chama kingine, bali mnaungana na kuwa kitu kimoja ni maneno mazuri ya kuiga mfano,” alisisitiza Mama Kikwete.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa aliwakemea watu wanaosema kuwa chama hicho hakijafanya  maendeleo, ambapo  alisema mtu anayesema  hivyo, sawa na kumdharau baba yake aliyempeleka shule.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top