Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali Yalikana Deni la Walimu



Sakata la madeni ya walimu limezidi kuchukua sura mpya baada ya serikali kusema haidaiwi na kwamba imebaini kuwapo kwa majina hewa ya walimu zaidi 4,000 yaliyowasilishwa kwa ajili ya malipo.

Imesema imegundua hivyo baada ya kufanya uhakiki wa deni la Sh. bilioni 19.6 lililowasilishwa na walimu baada ya kuwalipa madai yao kwa mara ya mwisho mwaka 2013.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, baada ya kuhakiki madeni hayo mwaka jana, serikali imegundua deni halisi inalodaiwa na walimu ni  Sh bilioni 5.6 tu.

Alisema endapo serikali isingefanya uhakiki wa deni hilo na kulilipa ingeingia hasara ya Sh. bilioni 14.

Alisema katika uhakiki huo, wizara hiyo imebaini kulikuwa na deni hewa kubwa la mwalimu mmoja wa Halmashauri ya Tunduru Mkoani Lindi Sh. milioni 500 na kwamba baada ya kuhakiki imegundua deni lake halali ni Sh. 500,000 tu.

Dk. Likwelile alisema kwa madeni ya mwaka jana, serikali imelipa walimu Sh. bilioni 5.6 baada ya kufanya uhakiki.

“Katika uhakiki tumebaini kuwapo udanganyifu wa fedha kwa walimu kujiongezea huku wengine wakidai deni la aina moja mara nne,” alisema.

Dk. Likwelile alitaja sababu za serikali kukataa kulipa baadhi ya madai ya walimu yaliyowasilishwa ni pamoja na kukosa vibali au vielelezo, madai mengine kuwa yameshalipwa, mishahara iliyowasilishwa kama madai yasiyo ya mishahara, baadhi ya walimu kutotambuliwa na halmashauri, baadhi ya walimu kutokuwa na madai katika majalada na makosa ya ukokotoaji na uandishi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top