SIRIKA
la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limezindua rasmi
kampeni yake mpya inayojulikana kama “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kampeni
ambayo ni endelevu inayolenga kuboresha huduma ya Maji safi na salama
maeneo yote ya jiji la Dar es salaam, pamoja na miji yote ya Kibaha na
Bagamoyo mkoani Pwani, huku ikimhakikishia mwanamke kumpunguzia adha ya
kutafuta Maji kutoka umbali mrefu.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa mtendaji mkuu wa Dawaso,
Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni hiyo ina malengo ya
kusogeza huduma ya Maji karibu kwa kuhakikisha inaongeza wigo wa huduma
ya Maji safi na salama kwa kujenga vituo takribani 18 ambavyo vitakuwa
vikitoa huduma ya Maji kwa wateja wake kwa muda wa saa 24 kupitia wakala
wake.
Katika
uzinduzi wa kampeni hiyo, Mhandisi huyo pia alitoa rasmi kibali cha
kuuza Maji kwa watu wote wenye visima na magari makubwa (Maboza) huku
akifanya usajili bure kwa wauzaji hao wa Maji na wamiliki wa visima
waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hizo, aliwataka wenye matanki kuacha
kuchota Maji sehemu ambazo sio rasmi kwani kwa kufanya hivyo
wanahatarisha afya ya watumiaji wa huduma hiyo.
“Ni
maarufuku kwa wenye matanki kuchota maji sehemu ambazo sio rasmi, sehemu
ambazo hazijasajiliwa, ni marufuku kuuza maji bila kuwa na leseni
kuanzia sasa kwani kwa kufanya hivyo mnahatarisha afya ya watumiaji wa
maji hayo” alisema Luhemeja.
Mhandisi
Luhemeja aliongeza kuwa, usajili huo utarahisisha upatikanaji wa huduma
ya Maji kwa kupeleka huduma hiyo mpaka kwenye makazi ya wananchi hao
huku ikiwahakikishia kupata Majisafi na salama hivyo kuondokana na
magonjwa ya milipuko yakiwamo kipindupindu.
“Uzinduzi
huu unalenga kupunguza usumbufu wa Maji majumbani pamoja kupunguza
kuuziwa Maji machafu yanayosababisha magonjwa ya mlipuko” alisema
Mhandisi Cyprian.
Kutokana
na wafanya biashara hao kuchoka Maji sehemu ambazo hazieleweki, uongozi
wa Dawasco umewatengea maeneo maalum ambayo watakuwa wakiyatumia kama
vituo vya kuchotea maji, baadhi ya maeneo hayo ambayo yatakuwa vituo vya
magari makubwa (maboza) kuchotea Maji ni kama Kimara, mbezi, kibamba
ccm, Bunju na namlandizi.
Mbali
na utoaji wa leseni na usajili wa magari, wamiliki na wauzaji wa magari
hayo, walitumia fursa hiyo katika kuchagua viongozi ambao watakuwa
wakiwasilisha taarifa za wauzaji na wamiliki hao wa magari ya Maji kwa
uongozi wa DAWASCO, huku uongozi wa Dawasco nao wakiwasilisha taarifa
zake kwa wafanya biashara hao kupitia viongozi hao waliochaguliwa.
Post a Comment