Pichani Ndugu Saidi Mwamende akimuliza swali Mhe: Jussa, (Hayupo Pichani)
Na
Swahilivilla. Blog Washington Waziri Majivuno wa Kusadikika alisema:
"Hekima ni kitu adimu kupatikana kwa mtu asiye na mvi...". Pia Waswahili
wanasema: "Akili ni nywele"
Mshitakiwa Karama aliipinga hoja ya Waziri Majivuno kwa kusema: "....Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima..."
Nimekuwa nikiyatafakari mafungu hayo matatu ya maneno ili kuona kama yana uhalisia wowote katika maisha yetu ya leo.
Hivi
majuzi swahibu yangu Said Mwamende alinipigia simu na mara tu baada ya
kuijbu, nilihisi sauti yake imejaa furaha, ndipo nikamwuliza
''umepandishwa cheo?" Akanijibu: "Hapana, bali nimekuwa nikifuatilia
siasa za Tanzania zinavyokwenda na nikakumbuka ule mkutano wa Mheshimiwa
Ismail Jussa alioufanya na Wanadiaspora hapa Washington.
Yale
aliyoyasema ndiyo yanayoendelea kutokea hivi sasa". Nikakurupuka
kuchakura maktaba yangu kuitafuta rekodi ya mkutano ule ili nijikumbushe
aliyoyasema Mheshimiwa Jussa. Baada ya kuiangalia tena, nikaona sehemu
ambayo Swahibu yangu Said Mwamende alimwuliza Mheshimiwa Jussa swali
ambalo lilihitaji mwono na mtazamo wa kina wa kisiasa: "Je, UKAWA,
tuseme, kwa upande wa chama chako wewe atakuwepo Mheshimiwa Lipumba, na
tuseme kwa upande wa CHADEMA Mzee wetu Mbowe. Watu hawa tayari
wameshagombea Urais.
Je
hamuoni kwa CCM kwa sasa hivi kuna hombwe la aina fulani? Kuna
Mheshimiwa Lowassa inawezekana kwamba hatogombea CCM kutokana na labda
hawatomtaka. Mnafikiriaje UKAWA kama mtamchukua yule Lowassa ili
mumuweke pale agombee?" Kwa ulimi wa fasaha kuliko wa Karama wa
Kusadikika, Mheshimiwa Jussa alilijibu swali la Bwana Mwamende ambaye ni
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania katika Jiji la Washington na
Vitongoji vyake (DMV), kwa kusema: "Katika siasa, wiki moja inaweza kuwa
muda mrefu sana".
Aliendelea
kwa kusema kuwa siyo Lowassa tu, anaweza kupitishwa Loawassa akaachwa
mtu mwengine mwenye ugomvi na Lowassa vilele. Kwa sababu CCM hivi sasa
siyo chama tena kinachowaunganishwa na itikadi. Kinachowaunganisha ni
Escrow na kwamba kila mmoja atapata mgao wake kiasi gani".
Mhe: Ismail Jussa akijibu swali la Saidi Mwamende (Hayupo pichani)
Katika
mkutano huo uliofanyika tarehe 28 Februari mwaka huu jijjini Washington,
Bwana Ismail Jussa, aliwathibitishia Wanadiaspora wa Tanzania nchini
Marekani pamoja na ulimwengu kwa ujumla kuwa Elimu ilipokuwa haijulikani
hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima, lakini
nadharia hiyo wakati wake umepita na hautorejea tena.
Post a Comment