Mh. Lowassa akihutubia mkutano huo wa kampeni
Mgombea
jubunge jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassary, akizikusanya kadi za
Wanachama wa CCM zilizorudishwa na kujiunga na Chadema, wakati wa Mkutano
wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini leo Oktoba
5, 2015
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA,
Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya
CHADEMA, Julius Kalanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika
kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini leo Oktoba 5, 2015
Wananchi
wa Monduli wakimpokea kwa shangwe, mpendwa wao ambaye ni Mgombea Urais wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward
Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini, leo
Oktoba 5, 2015
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA,
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa, wakishiriki tendo la kimila ya
Jamii ya Watu wa Kimasaai lililoongozwa na Malaigwanani, wakati akiwasili
kwenye Uwanja wa Polisi, Monduli Mjini, leo Oktoba 5, 2015
Picha ya juu na chini, Mh. Lowassa akihutubia mkutano huo wa kampeni
Mgombea
Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), anayewakilisha vuguvugu la UKAWA,
Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, wakionyesha
lundo la kadi za wanachama wa CCM wa Wilaya ya Monduli, waliozirudisha ili
kuungana na Watanzania wote kwenye harakati ya Mabadiliko, wakati
wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi,
Monduli Mjini leo Oktoba 5, 2015. Kulia ni Aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Monduli, Rubein Ole Kuney aliejiunga na Chadema.Picha na Othman Michuzi,
Monduli. (Picha na Othman Michuzi)
NA K-VIS
MEDIA
ULE msemo
wa Kiswahili usemao “mcheza kwao hutunzwa” umedhihirika leo wilayani Monduli,
baada ya mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
CHADEMA, akiwakilisha vyama vine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,
Mh. Edward Lowassa, ametua jimboni kwake “nyumbani” Monduli, na kuhutubia
mkutano mkubwa wa kampeni ambapo wanachama kadhaa wa CCM, wamerudisha kadi na
kujiunga na UKAWA.
Wanachama
hao wa CCM waliokihama chama hicho, waliongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Monduli, Reuben Ole Kuney.
Post a Comment