Jumuiya
ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa
karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika
kwa njia za amani na utulivu.
Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
Ama
kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha
nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii
mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo.
Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
Kwa
hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar,
kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na
kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha
Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano
isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.
ZADIA
pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao
juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,
ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao
wanaoishi nchini Marekani.
Aidha,
tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed
Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo
ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za
kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa
inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya
kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha
yao kwa jumla.
ZADIA
pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake
aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na
kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani
na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli
Tanzania ni kisima cha amani.
Na
mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote
kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya
nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu
haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata
kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki, Zanzibar.
Post a Comment