Na Ally Daud-Maelezo
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa vijana kutojihusisha na vitendo vya fujo katika kipindi hiki cha kampeni badala yake waelekeze nguvu na juhudi zaidi katika kujenga uchumi wa taifa.
Akiongea
katika mkutano uliowakutanisha NEC na wawakilishi wa vijana kutoka
mikoa mbalimbali nchini Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji mkuu Mstaafu wa
Zanzibar Mhe. Hamid Mahmoud Hamid (pichani) alisema kuwa vijana
wasitumike na vyama vya siasa kama kichocheo cha fujo .
“Vijana
kamwe msikubali kutumika kwa maslahi ya chama cha siasa ila tumieni
vizuri elimu yenu na upeo wenu wa kufikiri namna ya kujenga na
kuendeleza taifa”,alisema Jaji Hamid.
Naye
Mkurugenzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhan amesema kuwa wananchi
wanatakiwa kuheshimu sheria na kanuni za uchaguzi kwa mwaka huu wa
2015 ili kufanya uchaguzi kuwa haki na amani.
“
Natoa wito kwa wananchi wa Tanzania kuepuka kuingilia kazi za
watumishi wa Tume ya uchaguzi kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi
atapiga kura katika kituo alichojiandikisha ili kuepusha usumbufu “
alisema Bw. Ramadhan .
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi imeweka utaratibu maalum wa namna ya kutangaza
matokeo ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu kwa
ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani ambapo madiwani watatangazwa na
mkurugenzi wa NEC ngazi ya kata, Wabunge ngazi ya Jimbo na Rais
atatangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
Post a Comment