Wanasemina wakifatilia kwa karibu mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Wanasemina ya masuala ya Uchaguzi kanda ya ziwa wakiwa darasani.
Bi. Jescar Mongi kutoka tume ya uchaguzi hapa akionesha mfano wa utaratibu wa upigaji kura utakavyokuwa.
UCHAGUZI MKUU MAANDALIZI KANDA YA ZIWA YAENDELEA VIZURI
Na Atley Kuni- The Power of Media grew.
Wasimamizi waaswa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu
Imefahamika
kwamba maandalizi muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa
yanaendelea vizuri huku, waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa
uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba 25 mwaka
huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi
kumalizika.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya
taifa ya uchaguzi na kuhusisha Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi
wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi, na maafisa uchaguzi kutoka katika
mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Manju Msambya,
amesema watumishi hao wanayo dhima ya kuhakikisha zoezi la uchaguzi
linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Msambya
amesema nilazima dhamana waliopewa watumishi hao watambue ni muhimu
kwakua inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako taka
kuelekea kwa kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais.
“Ndugu wanasemina tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge
uwezo katika mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura,
kuhesabu, kujumlisha pamoja na kutangaza matokeo ya uchaguzi” hivyo
suala la umakini ni muhimu sana.
Msambya
amesema, kwakutumia uzoefu walionao watumishi hao katika mazoezi mbali
mbali ya kitaifa wataweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa hasa
ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki katika zoezi kama hilo kwa
mwaka 2010.
Awali
akimkaribisha kufungua semina hiyo Mratibu wa uchaguzi wa kanda ya ziwa
Deogratius Nsanzugwanko alisema tayari maandalizi kadhaa kuhusiana na
uchaguzi yamekwisha kamilika ikiwapo madaftari ya mikoa ya kanda ya ziwa
pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa tayari vimekwisha anza kusafirishwa
kwenda kwenye mikoa husika.
Kanda
ya ziwa inayoundwa na mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu
na Mara, ambapo kwa mkoa wa Mwanza pekee inakadiriwa kuwa na wapiga
kura 1,442,391 sawa na asilimia 103% ya lengo lililokuwa limewekwa hapo
awali na bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya kuandikisha wapiga kura
1,403,763.
Post a Comment