Mbunge
mteule wa jimbo la Mikumi kwa tiketi ya Chadema Josephu Haule maarufu
kama Profesa J amewashukuru wananachi wa jimbo hilo kwa kumpa ridhaa na
kuahidi kushirikiana na wananchi wote katika kuleta maendeleo ya jimbo
la Mikumi.
Akizungumza
na wananchi wa jimbo la Mikumi mbunge huyo mteule Profesa J amesema
jimbo la Mikumi lilisahaulika kwa miaka mingi huku wananchi wakiendelea
kukosa huduma bora za kijamii ambapo amaesema atahakikisha anaisimamia
rasilimali za jimbo la Mikumi ziwanufaishe wananchi wote.
Kwingineko
katika jimbo la Morogoro mjini viongozi wa vyama vya upinzani wameeleza
kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa madiwani katika kata za
Chamwino na mazimbu kutokana na uchaguzi wa kata hizo kugubikwa na
changamoto lukuki zikiwemo kuzalishwa vituo feki vya kupigia kura siku
ya uchaguzi.
Post a Comment