Watu
watatu wamefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na mashtaka
ya wizi wa kimtandao na kujipatia Sh4 milioni kwa njia ya udanganyifu.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kusajili namba za simu za uongo, huku wakifungua akaunti
ya benki ya NMB kwa jina la vyama vya Chadema na CCM wakitaka wachangiwe
fedha za kuendesha kampeni za Uchaguzi Mkuu
Wakili
wa Serikali, Castuce Ndamugoba aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Bony
Tefe (40), mkazi wa Mahina, Spridon Njunwa (38) mkazi wa Igoma, na
Briton Wilson (43) ambaye ni fundi cherehani na mkazi wa Bugando, Mwanza
Post a Comment