Afisa
Utumishi, Allan Mwela akikabidhi moja ya mizinga kwa mwanachama wa
kikundi cha wafuga nyuki kutoka kijiji cha Utosi kilichoko wilaya ya
Mufindi
Baadhi ya wafugaji nyuki wakisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela. (picha na Denis Mlowe.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesera akizungumza na wafugaji mara baada ya kukabidhi mizinga ya nyuki.
Mkuu wa wilaya Richard Kasesela akikabidhi moja ya mizinga 175 kwa mfugaji nyuki kutoka Kiwele.( PICHA NA NA DENIS MLOWE, MUFINDI).
NA DENIS MLOWE, MUFINDI
TIMU
ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana
na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) umetoa jumla ya mizinga ya
kufugia nyuki 350, kwa vikundi 16 vya wilaya ya Mufindi na Iringa
vilivyoko katika mkoa wa Iringa.
Akizungumza
wakati wa ugawaji wa mizinga hiyo iliyofanyika katika kata ya Sadan
wilayani Mufindi juzi, Afisa mradi wa LEAT kutoka Mufindi Jamal Juma
alisema lengo la mradi huo ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na
kuongeza kipato cha jamii kwa njia ya kufuga nyuki na kupanda miti.
Alisema
kuwa malengo mengine mahususi ya mradi huo ni kuleta ufanisi wa
kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na
kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali mara baada ya mauzo ya asali
iliyovunwa kupitia mizinga hiyo.Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa
mataifa machache yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili mathalani
misitu na wanyapori hivyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa mwananchi
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Juma
alisema kuwa kutokana na hali hiyo kuna changamoto mbalimbali za
usimamizi na uhifadhi zikiambatana na uchomaji moto ovyo, kuchoma
mkaa,ukataji miti uliokithiri na ujangiri mambo ambayo inasababisha
hasara kwa taifa.Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo husababisha
umaskini, kukauka kwa vyanzo vya maji kutoweka kwa uoto wa asili na
kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.
“
Mradi huu utasaidia sana jamii ya watu wa wilaya ya Mufindi walioko
katika vikundi vya ufugaji nyuki kuhakikisha unaboresha kipato kwa
kuendesha mafunzo ya ufugaji nyuki na uvunaji, upandaji miti,kusaidia
jamii kwa kuzipatia vitendea kazi vya ufugaji nyuki kama hivi ambavyo
leat imetoa kwa kusaidiana na USAID utasaidia kuondokana na changamoto
zote hizo endapo utafanyiwa kazi kwa umakini. “ alisema
Alisema
kuwa awamu ya kwanza ya mradi vimenufaisha vikundi 8 vyenye watu 22
vilivyoko katika vijiji vya Lugoda, Lutali, Igombalavanu, Uhimbila,
Mapogoro, Utosi, Tambalang’ombe, Kibada na Nyololo katika wilaya ya
Mufindi na vikundi 8 katika wilaya ya Iringa ambapo kila kikundi
kimepata mizinga 22 kama mtaji .
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufundi,Joika Kasunga katika hotuba yake
iliyosomwa na Afisa Utumishi, Allan Mwela amewaasa wananchi wanaokaa
pembezoni mwa misitu kuacha kufanya shughuli za uhalibifu wa msitu
ikiwemo uchomaji moto kwa ajili ya uwindaji shughuli za kilimo pamoja na
uchomaji wa mkaa.
Aidha
amewataka wananchi wa kuitunza vizuri misitu ili kuweza kuendelea
kupata mvua kwa wingi na kuondokana na mabadiliko ya hali ya hewa
yaliyopo kwa sasa kwani misitu inavyoathiliwa na wananchi kwa matumizi
ya kila siku na kusema kuwa chanzo cha misitu hiyo kuharibika ni
kutokana na wananchi wenyewe.
“Uhifadhi
wa misitu sio suala la mtu mmoja au kundi moja ila la watu wote hii
inatokana na ukweli kwamba madhara yatokanayo na uaribifu wa mazingira
hayana mipaka na humpata kila mtu hivyo ni wajibu wa kila mtanzania
kushiriki katika kulinda maliasili” alisema .
Aliwapongeza
Leat kwa kuweza kuwasadia wajasiliamali walioko katika vikundi vya
kuondokana na umaskini kwa njia ya ufugaji wa nyuki.
Post a Comment