Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Majambazi yateka mabasi ya abiria Singida

Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameyateka magari matano ya abiria na kuwapora mali mbalimbali zenye magari matano ya abiria na kuwapora mali mbalimbali zenye thamani ya Sh1.3 milioni. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4 usiku eneo la Iguguno, wilayani Mkalama. 

Alidai kuwa watu hao wakiwa wamebeba silaha za jadi, waliyateka magari hayo na kisha kuwajeruhi madereva kabla ya kufanya uporaji huo. 

Kamanda huyo aliwataja madereva waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Yasini Shemboko (40) mkazi wa Tanga, Ally Mchoba (40) na Abood Juma (24) wote wakazi wa Dar es Salaam, Anold Adamu (23) mkazi wa Shinyanga na Mathias Rameck (44) mkazi wa Mwanza. 

Alisema majeruhi hao walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida walikopatiwa matibabu na kuruhusiwa. 

Kamanda Sedoyeka alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya utekaji wa magari kwa kuwa wanaishi nao. 

Alisema mpaka sasa hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi wanaendelea na msako. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top