Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWSS ... ACT WAZALENDO WATOA TAMKO KALI



MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA ACT-WAZALENDO KUFUATIA KIKAO CHAKE KILICHOFANYIKA JUMAMOSI 13 FEBRUARI 2016KATIKA HOTELI YA KAGAME JIJINI DAR ES SALAAMKamati Kuu ya Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo)ilifanya kikao chake cha kawaida siku ya Jumamosi tarehe 13 Februari 2016 katika Ukumbi wa Hoteli ya Kagame Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ilijadili, kutolea maoni na kuazimia mambo yafuatayo yanayohusu chama na Taifa kwa ujumla.1. Kamati Kuu ilijadili na kuzingatia hali ya kisiasa nchini na kutolea maoni mambo yafuatayo:b. Kamati Kuu iliwapongeza wananchi na Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa amani kwa upande wa Jamhuri Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Kamati Kuu iliaani kitendo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar za kuvuruga zoezi la kukamilisha kujumlisha matokeo ya kura zilizopigwa katika uchaguzi huo.c. Kamati Kuu ilipokea na kujadili utendaji wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli katika siku zake 100 madarakani na kuzingatia yafuatayo:i. Kamati Kuu imetambua jitihada za serikali ya Dk Magufuli katika kupambana na rushwa na ufisadi nchini kupitia dhana ya kile anachokiita ‘kutumbua majipu’. Hata hivyo, Kamati Kuu imezingatia kuwa, pamoja na juhudi hizi, bado hali ya maisha ya wananchi imeendelea kuwa ngumu kama inavyothibitishwa na kuendelea kupanda kwa bei yabidhaa muhimu kwa maisha ya binadamu kama vilesukari, mchele, na mafuta ya kula. Aidha, pamoja nabei ya mafuta kuendelea kushuka kwa kasi katika soko la mafuta duniani, bei ya mafuta hapa nchini imeshuka kwa kiwango kidogo kisicholingana na kiwango cha kushuka katika soko la dunia.ii. Pamoja na kwamba chama chetu kinaunga mkono juhudi za kuwachukukia hatua za kinidhamu watumishi wa umma wenye tuhuma za rushwa na ubadhirifu wa mali za umma, Kamati Kuu imesisitiza kuwa juhudi hizo ziendelea kuchukuliwa kwa kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, utawala bora na utu. Aidha, serikali ya Rais Magufulibado haijaanza kujishughulishana kubadili mifumo iliyoasisi rushwa na ufisadi nchini, ikiwemo: kubadilimikataba ya kinyonyaji ya raslimali, kufuta posho zamakalio (sitting allowances) katika mfumo wa utumishi wa umma ikiwemo Bunge; kuachana na matumizi ya magari ya anasa (mashangingi); kupiga marufuku uagizaji wa sukari nje; kuifanyia mabadiliko TAKUKURU.iii. Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa Rais Magufuli hajalipa kipa umbele suala la Katiba Mpyaambayo ndiyo imekuwa ajenda kubwa kwa miaka mingi sasa. Kamati Kuu imemkumbusha Rais ahadiyake Bungeni kuanzisha mchakato wa kukamilisha uandikaji wa Katiba Mpya.2. Kamati Kuu imepokea na kujadili hali ya kisiasa katika visiwa vya Zanzibar na kuzingatia na kuazimia yafuatayo:a. Kama Kuu imeendelea kusisitiza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Ndugu Jecha Salumu Jecha, hakuwa na uhalali wa kisiasa,kikatiba na kisheria kufuta zoezi lililokuwa linaendelea la kuhesabu kura mnamo tarehe 28 Oktoba 2015. Kamati Kuu imezingatia pia kuwa, mbali na Chama cha Mapinduzi, waangalizi wote wa uchaguzi wa ndani na nje, pamoja na Jumuiya ya Kimataifa, ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki,wametamka bayana kwamba uchaguzi wa Zanzibarulifanyika katika mazingira ya haki, huru na demokrasia na matokeo ya uchaguzi huo yalizingatia utashi na matakwa ya wapiga kura wa Zanzibar. Kwa kuzingatia haya, Kamati Kuu imeazimia yafuatayo:i. Kupinga marudio ya uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi 2016, na kwamba Chama chetu cha ACT-Wazalendo hakitashiriki katika uchaguzi huo kama utaendelea kama ulivyopangwaii. Kutoa wito maalumu kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuchukua hatua stahiki za kiuongozi katika kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzaibar, na kuacha kutoa vitisho vya kidola katikakushugulikia tatizo hili. Kamati Kuu imemtaka Rais Magufuli kutumia mamlaka aliyepewa kikatiba kuhakikisha kwamba Umoja na Amani ya Taifa inaendelea kuimarika nchini kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, utawala wa sheria na utawala bora.iii. Kamati kuu ya ACT-Wazalendo inahimizi kuwa madiwani na wawakilishi walioshinda na kutangazwa rasmi na ZEC katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25/2015 watambuliwe na waanze kuwatumikia wananchi.iv. Kamati Kuu imeendelea kuhimiza wadau wote muhimu katika siasa za Zanzibar kuendelea kufanya mazungumzo katika kutatua mkwamo wa kisiasa. Kamati Kuu haiamnini kwamba suluhu ya kudumu kuhusu changamoto za kisiasa Zanzibar zitapatikana kwa ubabe na matumzi ya nguvu za kidola.3. Kamati Kuu imepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya uchaguzi wa chama na utendaji wa chama baada ya uchaguzi na kuzingatia yafuatayo:a. Kamati Kuu imewapongeza wananchi waliojitokeza kupiga kura na kukiunga mkono chama na hata kufanikiwa kumpata mbunge mmoja, madiwani 41 katika mikoa mbalimbali, na kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujijib. Kamati Kuu imepitisha azimio maalumu la kumpongeza Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe kwa kazi kubwa anayoifanya ya kibunge kwakushirikiano na wabunge wenzake wenye uzalendo na wanaozingatia maslahi mapana ya Taifa.c. Kamati Kuu imepitisha taarifa ya mapato na matumizi katika uchaguzi mkuu ambapo chama kilipokea na kutumia shilingi 656,625,0000/=.d. Kamati Kuu imevipongeza vyombo vya habari kwa kazi kubwa waliofanya katika kuwaelimisha wananchi kuhusu uchaguzi mkuu na kwa kufanya kazi kwa weledi na bila ubaguzi4. Kamati Kuu imejadili na kupitisha Mkakati wa Chama kwa kipindi cha miaka mitano 2016-2020. Mkakati huu unalenga kukiimarisha chama katika maeneo matano yafuatayo:i) Kuimarisha safu ya uongozi na watendaji katika ngazi zoteii) Kuimarisha mfumo wa mawasiliano ya ndani na kwa ummaiii) Kuibua na kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi kwa kuwashirikishi wananchiiv) Kuimarisha mahusiano na vyombo vya habariv) Kujiandaa kikamilifu na kimkakati kwa chaguzi zaserikali za mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, na chaguzi ndogo zitakazojitokeza.5. Ili kutekeleza kikamilifu Mkakati wa Chama, pamoja na hatua zingine, Kamati Kuu imeziunda upya Kamati za chama makao makuu kama ifuata


vyo:i) Kamati ya Fedha na Miradi ya Kujetegemeaii) Kamati ya Utafiti, Sera na Mipangoiii) Kamati ya Uadilifu, Ulinzi na Usalama wa Chamaiv) Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Njev) Kamati ya Itikadi, Mawasiliano na Uenezivi) Kamati ya Maendeleo ya Jamiivii) Kamati ya Mafunzo na Chaguziviii) Kamati ya Wabunge na Uendeshaji wa Serikali za Mitaa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top