Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ELIMU YA KIDATO CHA TANO NA SITA KUTOLEWA BURE

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussein J Ruhava ametangaza kutoa elimu bure kwa manispaa hiyo kwa kidato cha tano na sita, na gharama zake zitalipwa kutokana na mapato yanayotokana na minara ya simu katika manispaa hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, na kueleza kuwa jambo hilo limeshapitishwa kwenye bajeti ya halmashauri ya manispaa.

"Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ametangaza rasmi kwamba elimu ya kidato cha tano na cha sita katika manispaa itakuwa bila malipo. Manispaa itafidia mapato ya ada hizo kwenye mashule kupitia makusanyo yake ya ndani yanayotokana na tozo za minara ya simu", aliandika Zitto Kabwe.

Pamoja na hayo mbunge huyo ametoa taarifa kuwa Meya huyo amekataa kununuliwa gari ya Tshs milioni 150, na kuelekeza fedha hizo kwenda kwenye matumizi ya maendeleo na haswa miundombinu ya mji.

Pia Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa serikali za mitaa zina changamoto kubwa katika kukusanya mapato na matumizi, hivyo kuna haja ya kuingiza mfumo wa matumizi ya sayansi na teknolojia katika kazi hiyo.

"Serikali za Mitaa zina changamoto kubwa ya makusanyo ya mapato na matumizi mabaya, matumizi ya teknolojia yanahitajika sana kudhibiti upotevu wa mapato na kuepuka matumizi mabaya", aliandika Zitto Kabwe.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top