Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAJAMBAZI YAUA WANNE


Wafanyabiashara wanne wa Tanzania wameuwa kwa kupigwa risasi kisha kuchomwa kwa vitu vyenye ncha kali nchini Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo lilitokea usiku wa Jumatatu iliyopita katika machimbo ya dhahabu, Kijiji cha Mtoro Mtupweshi Kamprigando.

Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Salum Mfanga (44) Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Yusuph Twalibu (34) na Mariam Ramadhani (30) wakazi wa Tanga na Hamisi Mkapira (40) wa Morogoro.

Kamanda huyo alisema kifo cha Mariam ambaye alifanikiwa kujiokoa, kilisababishwa na kukosa huduma ya haraka baada ya kuvunjika mguu.

Kamanda huyo alisema wafanyabiashara hao walivamiwa na majambazi waliokuwa na risasi pamoja na mapanga katika vibanda vya kubadilishia fedha nchini humo.“Miili ya wafanyabiashara hao ililetwa na ndugu zao ambao wanaishi Msumbiji,” alisema.

Wakizungumzia tukio hilo, Said Mfanga na Dotto Ramadhani ambao ni ndugu wa marehemu hao walisema baada ya kuwaua, majambazi hao waliwapora fedha pamoja na mabegi yao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top