Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene ameonya kuwa atawachukulia hatua watendaji wa Manispaa ya Kinondoni watakaobainika kutoa hati za nyumba zilizojengwa katika soko la Tandale kinyume cha utaratibu.
Simbachawene alitoa onyo hilo jana aliposhiriki kufanya usafi na wafanyabiashara wa soko hilo ikiwa ni sehemu kuadhimisha siku hiyo kila mwisho wa mwezi.
Alisema hiyo ni mara yake ya pili kufanya ziara ya katika soko hilo, lakini kila akifika anapewa malalamiko ya mipaka ya soko hilo.
Alisema manispaa hiyo inadai katika nyaraka zake soko hilo halina hati, hivyo siyo halali.
“Kila nikija hapa kilio ni hiki hiki, pia haingii akilini eti nyumba zilizoko hapa zina hati halafu soko hili halina hati,”alisema Simbachawene.
Alisema endapo soko hilo litakuwa na hati litaweza kutoa huduma zake kwa ufanisi kwani litaboreshwa na kuongezewa uwezo kama masoko mengine makubwa nchini.
Simbachawene alisema ujio wake wa awamu ya pili sokoni hapo, umemsaidia kutembelea maeneo ya soko na kubaini kuwapo alama ya jiwe, lakini cha kushangaza halina hati.
“Nimemuagiza mkuu wa wilaya akutane na viongozi na soko na wazee wa eneo hili ili kubaini ukweli,” alisema.
Mwenyekiti wa soko hilo, Mohamed Mwekya alimuhakikisha Simbachawene kumpa ushirikiano katika suala hilo ili lipatiwe ufumbuzi na hatimaye soko lipige hatua za kimaendeleo
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
Kwa Undani12 hours ago
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment