Waziri wa zamani wa Kilimo, Chakula na Ushirikia Stephen Wasira amekosoa muundo wa wizara za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, akidai kuwa hana uhakika kama inabana matumizi kama inavyoelezwa akilinganisha na uliopita.
Wasira ambaye alichukua fomu za kuwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka jana, amesema kuwa kuna baadhi ya wizara zimepewa jina moja lakini kimantiki kuna wizara mbili ndani yake.
“Kwa mfano, ipo wizara moja inaitwa Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa, Utumishi na Utawala Bora. Lakini ina mawaziri wawili. Waziri mmoja anasimamia utumishi na utawala bora na mwingine anasimamia tawala za mikao na serikali za mitaa, sasa hiyo ni wizara moja?” Wasira anakaririwa katika mahojiano maaalum aliyofanya hivi karibuni na gazeti la Mwananchi.
“Kila wizara ina katibu mkuu wake, kwa hiyo ni wizara mbili zimepewa jina moja. Kwa hiyo mimi nikijumlisha naona wizara 19 na mawaziri 19,” aliongeza.
Wasira alisema kuwa ingawa hana uwezo wa kupiga mahesabu na kuthibitisha kutumia wizara zote endapo muundo huo wa baraza la mawaziri umebana matumizi au la, anaweza kutumia wizara mbili ili kutoa picha ya jambo hilo.
“Hapa sina calculator, lakini naweza kutoa maoni kwenye wizara mbili, moja ya kilmo ninayoijua zaidi, ambayo imeunganishwa na mifugo na uvuvi ina na ina makatibu wakuu watatu,” mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.
“Mifugo ina katibu mkuu wake, kilimo ina katibu mkuu wake na uvuvi ina katibu mkuu wake. Sasa unahitaji calculator ili kujua kama gharama zimepungua, kwa sababu huko nyuma kulikuwa na mawaziri wawili na makatibu wakuu wawili,” aliongeza.
Wasira amekuwa waziri wa tatu wa serikali iliyopita waliojitokeza kukosoa muundo wa wiziai za Serikali ya Awamu ya Tano kwa ulinganifu na ubanaji matumizi, baada ya Bernard Membe na Dk. Makongoro Mahnga kujitokeza hadharani kukosoa miezi michache iliyopita.
Katika hatua nyingine, Wasira alimshauri Rais Magufuli kuitoa idara ya umwagiliaji kutoka Wizara ya Maji na kuirudisha Wizara ya Kilimo ilipokuwa awali kwa kuwa umwagiliaji ni sehemu ya kilimo.
Post a Comment