Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI UMMY MWALIMU AWASHUKIA WANAOTOA HUDUMA ZA AFYA KINYUME CHA SHERIA


Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyataka Mabaraza na Bodi za kitaalamu za masuala ya afya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wataalam na vituo vinavyotoa huduma za afya kinyume cha Sheria.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo alipokuwa akizindua Baraza la Optimetria, Baraza la wataalamu wa Radiolojia pamoja na Bodi ya Maabara binafsi leo jijini Dar es salaam.

Alisema kisheria Mabaraza na Bodi za Kitataalam ndivyo vyombo vinavyofuatilia ubora wa huduma za Afya pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwaepuka watoa huduma batili wasiokuwa na utaalam na ujuzi wala kukidhi vigezo vya utoaji huduma vilivyowekwa kisheria. 

“Siku hizi kumekuwa na matumizi makubwa ya vyeti vya kugushi vikiwemo vya vituo vya kutolea huduma na wataalamu, watu wasio na taaluma wanatoa huduma kinyume na sheria hivyo Mabaraza na Bodi  mna mamlaka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu,” Alisema Waziri Ummy.

Aidha, alisema kuwa Serikali haitasita kuyachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuvunja Bodi au Mabaraza yatakayoshindwa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika sheria iliyohusika kuyaanzisha.

Aliyataka mabaraza hayo kuhakikisha kuwa yanatoa Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na ufahamu kuhusu huduma bora za afya zitolewazo na wataalamu  husika.

“Wananchi wakielimishwa wataepuka  watoa huduma batili wasiokuwa na utaalamu na ujuzi hivyo mabaraza na Bodi vinapaswa kuhakikisha mambo haya hayatokei  kwani vinauwezo mkubwa wa kufuatilia masuala haya kwa mujibu wa Sheria”alifafanua Waziri Ummy.

Akizungumza kuhusu utendaji kazi wa wataalamu hao Waziri Ummy amewataka wataalamu hao kujiendeleza kielimu kwani utaalamu bila kuwa na ujuzi ni butu hivyo suala la elimu lipewe kipaumbele.

Mbali na hayo Waziri ameitaka Mabaraza na Bodi kuhakikisha wataalamu wote, vifaa na vitendanishi vinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top