Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ASKARI POLISI AVUNJWA MGUU

Gari lenye namba za usajili T684 AYJ likiendeshwa na Emmanuel Charles Kazungu(43) mkazi wa Kitangiri limeacha njia katika eneo la kanisa katoliki Shinyanga mjini barabara ya Uhuru na kuwaparamia watembea kwa miguu akiwemo askari polisi H.4515 PC Geofrey ambaye amevunjika mguu wa kushoto.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo /siku ya mkesha wa pasaka majira ya saa nane usiku,ambapo mbali na kumjeruhi askari huyo pia watu wengini watano wamejetuhiwa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyang ACP Dismas Kisusi Kamanda Kisusi amewataja majeruhi wengine kuwa ni Majid Abdul(25)mkazi wa Kizumbi,Mashaka Juma (25) mkazi wa Katunda,Joseph Shija(22) mkazi wa viwanja vya Mwadui,Tendea Lutema(25) mkazi wa Old Shinyanga na Idd Magembe(30) mkazi wa Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva na tayari jeshi la polisi linamshikilia dereva huyo kwa hatua zaidi za kisheria.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top