Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINACHOENDELEA SAKATA LA KUPIGWA DAKTARI

Kufuatia tukio la ndugu wa mgonjwa  kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara,Henry Mwaibambe (Pichani) amesema hadi sasa watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya Mkoa wamekamatwa usiku wa kuamkia jana wakitoroka nchini huku wengine 3 wakiendelea kusakwa.

Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi

Jana, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliweza kufika Hospitalini hapo na kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama kwa watumishi hao wa Afya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top