Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mhe. William Lukuvi amesema amesema ofisi yake imebaini watu 200 waliodhululimiwa viwanja watarudishiwa na kuwataka kufika Wizarani ili kuhakiki nyaraka za umuliki wa viwanja vyao.
Kati ya hati zilizotolewa nchini zaidi ya Milioni moja na Laki Mbili Asilimia 75 ya hati zote zinatoka Dar es salaam kutokana na kutofuata sheria za Ardhi zinavyoelekeza.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi nchini Mhe.Wiliam Lukuvi ametyoa kauli hiyo leo alipokutana na Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii waliofika ofisi za wizara hiyo kwa lengo la kuhakikisha na kujua namna ya watanzania wanavyopatiwa huduma mbalimbali za ardhi hasa katika kutoa maamuzi na haki.
Mhe.Lukuvi amesema ofisi yake imeshagundua watu zaidi ya 200 ambao wamedhulumiwa viwanja vyao na wote waliodhulumiwa na Ofice yake imehakiki watawarudishia viwanja vyao sio zaidi ya mwezi wa sita mwaka huu na wote waliodhulumiwa wafike wizarani na vielelezo vyao vyote.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii Eng.Atashasta Nditiye amesema bado kuna mkanganyiko mkubwa wa wizara hiyo na Halmashauri nchini kutopeana kikomo cha majukumu yao na kusababisha migogoro ya Ardhi kuendelea kuwepo na uboreshaji wa huduma ya Tehama ili kuhakikisha watanzania wanaishi kwa amani kwenye ardhi zao.
Kwa upande wa wananchi waliofika wizarani hapo kwa ajili ya kuhudumiwa wamesema wanaiomba serikali kuharakisha utatuzi wa matatizo ya ardhi kwa uharaka bila kubagua.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Kwa Undani13 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo6 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment