Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MOTO WATEKETEZA NYUMBA TABATA


Dar es Salaam. Mshtuko umetokea jana katika mtaa wa Mtambani, uliopo Tabata jijini hapa baada ya kuzuka kwa moto ghafla na kuteketeza nyumba yenye maduka ya biashara na vyumba vya makazi, huku wahusika wote wakiwa nje ya maeneo hayo.

Mmoja kati ya majirani wa eneo hilo, Mathias Wambura alisema moto huo ulianza saa 11:00 jioni na baada ya nusu saa gari la zimamoto lilifika kwenye eneo la tukio.

Alisema juhudi za uokoaji wa awali zilianza kutolewa na majirani, lakini hazikufanikiwa.

Mmiliki wa nyumba huyo, Teobad John alisema chanzo cha moto huo hakijulikani licha ya siku za nyuma kuwapo kwa tatizo la mita ya luku, lakini tatizo hilo lilimalizika kwa kufanyika matengenezo.

John alisema nyumba hiyo yenye vyumba vinne, ilianza kuungua kwenye moja ya vyumba vya wapangaji na moto kusambaa kwenye maeneo mengine.“Siwezi kujua kama mpangaji huyo alikuwa anatumia gesi chumbani kwake,” alisema.

Alifafanua kuwa maduka mengine manne yalikuwa yamepangishwa kwa ajili ya kufanyia biashara kwa wapangaji wa huduma za chakula, tigo pesa, mafundi simu na saluni ya kiume, ambao walikuwa wamefunga maduka yao kabla ya moto kuanza kuwaka.

Alisema nyumba yake imeteketea ikiwa na thamani inayokadiriwa kufikia Sh18 milioni na hakuwa ameikatia bima.

John alisema baada ya moto kutokea maofisa wa Tanesco waliwahi kufika na kuzima umeme.

“Wapangaji wote hawakuwapo na wamejaribu kupewa taarifa tu kila mmoja, wanakuja,wengine walikuwa kazini na wengine siwezi kujua walikuwa wapi,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top