Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKURUGENZI TANESCO ASHINDA KESI ... AACHIWA HURU

Mhando
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando (kushoto) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Jana , ambapo alisomewa shitaka la matumizi mabaya ya madaraka. (Picha na Maktaba)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mkewe Eva Mhando na mtoto.
Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, hivyo kulingana na ushahidi walioutoa mahakamani, umeonyesha dhahiri kwamba hawana hatia na wameachiwa huru.
Kesi yao imesomwa na Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema.
Wakati huo huo, Wakili wa Serikali aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, Leonard Swai kwa njia ya simu amesema rushwa iliyopo mahakamani inatisha na serikali inatakiwa kuchukua hatua.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top