Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MUHONGO AWAPA MASHARTI MAGUMU TANESCO ... LA SIVYO ...

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa masharti matatu kwa mameneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) ili kulinda vibarua vyao.

Akizungumza juzi na mameneja wa wilaya, mikoa na kanda zote nchini, Profesa Muhongo alisema utendaji wao ndiyo utakaowafanya waendelee kuwapo kazini.

Alisema kila baada ya miezi mitatu itakuwa ikifanyika tathmini ya kuangalia utendaji wao.

Miongoni mwa masharti aliyowapa ni kuongeza mapato na idadi ya wateja wanaounganishiwa umeme katika maeneo yao.

Sambamba na hilo, mameneja hao watatakiwa kubunifu njia mathubuti za kutatua matatizo ya umeme yanayojitokeza.

“Tutaanza kuwapima kwa idadi ya watu wanaowaunganishia umeme katika meneo husika, kinyume na hapo watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe,” alisema Muhongo.

Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji aliwahakikishia Watanzania kuwa vifaa vinavyohitajika kuwaunganishia umeme vipo vya kutosha.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top