Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MAGHEMBE AWA MBOGO

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametoa miezi miwili kwa wafugaji wanaochungia N’gombe katika hifadhi ya Kigosi Muyowosi wawe wametoa mifugo yao kwa hiari katika hifadhi hiyo ifikapo juni 15 mwaka huu.

Akizungumza na wafugaji wa Kanda ya Ziwa ambao baadhi yao mifugo yao imekamatwa Waziri Maghembe amesema ni kweli wafugaji hawana maeneo ya kuchunga lakini hakuna mwananchi atakayevumilia ukame na uharibifu wa mazingira unaoweza kutokea kutokana na kuacha hifadhi za misitu zikatumika bila utaratibu.

Aidha Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amesema tayari Wizara yake imeanza mchakato wa kutenga maeneo maalumu ya ufugaji ili kuondoa migogoro iliyopo pia amewataka maafisa wanyamapori kuwa na utu wanapoikamata mifugo tofauti na taarifa wanazozipata ya kuwa kuna baadhi ya maafisa hao huzipiga N’gombe risasi wanaposhindwa kuelewana na wafugaji.

Naye Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko amesema malalamiko ya kuonewa wafugaji yamekuwa ya muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi jambo linalowasababishia umasikini wananchi wa Bukombe kutokana na baadhi ya maafisa wanyamapori kuchoma nyumba za wananchi na kutaifisha mifugo kinyume na utaratibu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top