Mwalimu huyo anakabiliwa na tuhuma za kushawishi rushwa ya ngono na kujaribu kupewa wakiwa kwenye nyumba hiyo.
Inadaiwa kuwa alikuwa akiomba rushwa hiyo kwa mwanamke ambaye Februari 17 alifika shuleni kumuombea uhamisho mdogo wake wa kiume wa darasa la sita wa kuhamia Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Joshua Msuya alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa 10.00 jioni
Msuya alidai kuwa mwanamke huyo alibembeleza kwa muda mrefu apewe uhamisho huo, lakini mwalimu huyo alimpa sharti kwamba wafanye mapenzi kwanza ili ampatie uhamisho huo.
Katika tukio jingine, Takukuru Mkoa wa Dodoma inawashikilia Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Bahi na mthamini wa wilaya hiyo kwa tuhuma za kujenga daraja chini ya kiwango.
Pia, Takukuru inamshikilia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Masons Eng Co.Ltd kwa kujenga daraja jilo lililopo barabara ua Kigwe mnadani kinyume na mkataba.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa baada ya taasisi yake kupata taarifa na kujiridhisha kuwa, makosa yaliyotendeka ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
Kuhanga alisema watumishi hao walitenda makosa hayo wakijua ni kinyume cha maadili, ikiwamo kuiibia Serikali na kuitia hasara katika ujenzi wa mradi huo.
Alisema hivi sasa wanafuatilia kila mradi unaoendelea.
Alisema watumishi hao wamekamatwa kipindi cha utendaji kazi wa miezi mitatu mitatu waliyojiwekea Takukuru, ambako kwa wakati huo pia walifanikiwa kumkamata na kumfikisha mahakamani Ofisa wa TRA, Flavian Chacha kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh1.5 milioni.
“Mfano Mizani ya Nala waliweza kukusanya Sh1.9 milioni kwa siku 10 kabla hatujakwenda, tulipotia timu walipata milioni 5.3 wakati stendi ya mkoa walikusanya milioni 2.8, tulipofika wakakusanya milioni 4.1,” alisema.
Post a Comment