Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI KIBOKO ... AAMURU VIGOGO KUTUMIA MABASI BADALA YA MASHANGINGI KWENDA BUNGENI, DODOMA

Rais John Pombe Magufuli ameagiza kuwa Wakurugenzi wote wa Wizara mbalimbali watakaohudhuria vikao vya kamati za bunge Mjini Dodoma, watasafiri kwa mabasi badala ya magari yao "mashangingi" ya serikali kama ilivyozoeleka.


Katika utaratibu huo mpya kila Wizara itakodi basi (Coaster) kwa ajili ya kusafirisha Wakurugenzi hao kwenda Dodoma kwenye vikao vya bunge ili kutoa msaada kwa wizara zao pale wanapohitajika kufanya hivyo. Rais amefikia maamuzi haya ktk jitihada za kupunguza gharama za mafuta na posho za madereva wa wakurugenzi wanaposafiri kuelekea Dodoma. 

Hata hivyo Wakurugenzi hao hawazuiwi kusafiri kwa magari yao binafsi (personal) kwa kujilipia gharama zote wao wenyewe ikiwa watataka kufanya hivyo. Katika utaratibu huu mpya inamaanisha kuwa viongozi wa wizara watakaosafiri kwa "mashangingi" kuelekea Dodoma ni Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu mkuu tu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top