Mkuu wa mkoa wa dsm Paul Makonda ameitaka mamlaka ya Usafirishaji wa nchi kavu na majini Sumatra, Halmashauri za jiji la dar es salaam pamoja na jeshi la Polisi kuangalia Upya sheria zinazowakataza waendesha bodaboda kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam katika kudhibiti matukio ya uhalifu na Uvunjaji wa sheria za barabarani.
Akizungumza katika mkutano uliwajumuisha waendesha bodaboda jiji la dsm kuangalia changamoto,matukio ya uhalifu wa kutumia silaha hususan kwa wahalifu wanaotumia bodaboda pamoja na ajali za barabarani Bwana Makonda amesema mkutano wa pamoja kujadili na kusimamia sheria hizo lazima uwashirikishe wahusika.
Aidha katika mkutano huo Bw,Makonda ameahidi kutoa pikipiki 5000 ambazo madereva watakopeshwa kwa kutanguliza laki mbili tu kutoka kwa wafadhili waliojitokeza huku akiwataka kuunda kamati na vikundi vitakavyotambulika pamoja na kusajiliwa upya kwa pikipiki zilizopo ili kuzitambua zinazojihusisha na uhalifu.
M/kiti wa muda wa waendesha bodaboda akizungumza katika mkutano huo ameainisha kero mbalimbali zinazowakabili waendesha bodaboda.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam amewahamaisha watumishi wa idara zote leo saa nne usiku kuangalia kituo cha Channel Ten ambapo wananchi watazungumza moja kwa moja kuelezea kero zao kwa mkuu wa mkoa ili wakuu hao wa idara wazifanyie kazi mara moja.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
Alfajiri8 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo8 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-



Post a Comment