SERIKALI imesema bajeti ya dawa kwa mwaka ujao wa fedha wa 2016/17 ni zaidi ya mara tatu ya bajeti ya mwaka wa fedha uliopita, lengo likiwa ni kuondoa tatizo la dawa na vifaa tiba kwenye hospitali,vituo vya afya na zahanati pamoja na kuweka utaratibu kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya na Mfuko wa Afya ya Jamii kupata dawa kwenye maduka ya MSD.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema haya jijini Mbeya, wakati akizinduzi dula la MSD pamoja na Ghala la kisasa la kuhifadhia dawa, ambalo litahudumia mikoa ya nyanda za juu kusini, huku akidai kuwa uanzishwaji wa maduka hayo haukusudii kuuwa maduka ya dawa ya watu binafsi, isipokuwa yatajifunga yenyewe kwa kuwepo kwa dawa zote kwenye maduka hayo, nakwamba wafanyabiashara hao wanatakiwa kufanya biashara nyingine na si zinazogusa maisha ya watu.
Aidha Waziri huyu amesema wapo baadhi ya watumishi wa afya ambao siyo waaminifu wanaihujumu serikali kwa kuuza dawa, ambapo ameiagiza serikali ya mkoa kufanya msako ili kubaini maduka ya watu binafsi yanayouza dawa za serikali na kuwachukulia hatua.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema lengo la kufungua maduka hayo ni kurahisisha upatikanaji wa dawa.
Loading...
Post a Comment