Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Hatua hizo zimetangazwa jana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, wakati akitoa taarifa kwa wabunge ya ukomo wa bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jana Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mpango amesema kati ya hatua muhimu watakazochukua ni pamoja na kufanya marekebisho ya sheria ya manunuzi ya Umma ili kuziba mianya ya upotevu wa fedha katika manununuzi na kuhakikisha yanawiana na thamani ya fedha itakayotumika.
Waziri huyo wa fedha amesema hatua nyingine ni kukamilisha ni mchakato wa kuziunganisha halmashauri zote nchini kwenye mfumo wa malipo ya kibenki ili kuongeza udhibiti wa matumizi ya fedha za umma na kufikisha malipo kwa wakati.
Aidha Dkt. Mpango amesema hatuna nyingine muhimu pia ni kuhakikisha , wizara na idara zinazojitegemea, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa zinatumuia mfumo wa malipo wa serikali (IFMS), ili kuepuka malimbikizo ya madai.
Post a Comment