Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo ametoa mchanganuo wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, ambayo wabunge wote walikuwa wanaijadili siku ya leo.
Katika ukurasa wake wa facebook Mh. Zitto kabwe ametoa mchanganuo huo wenye vyanzo vya upatikanaji wa fedha hizo, huku akisema kiasi kamili cha bajeti hiyo ni kizuri na chenye kuleta matumaini.
“Bajeti ya mwaka 2016/17 ni tshs 29.5 trillions,TRA watakusanya tshs 17.8 trilioni, mikopo itachukuliwa tshs 7.5 trilioni na misaada ya wafadhili 3.6 trilioni, matumizi ya kawaida tshs 17 trilioni na Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni. Bajeti ya tshs 29.5 trilioni ni hatua kubwa sana”, aliandika Mh. Zitto Kabwe.
Pia Mh. Zitto ameweka wazi kuwa serikali ina mpango wa kukopa kiasi cha shilingi trilioni 2.1, kutoka nje ya nchi, mkopo ambao utakuwa na masharti ya kibiashara.
Pamoja na hayo Zitto Kabwe amesema kitendo cha serikali kutaka kurasimisha sekta zisizo rasmi itasaidia kukuza pato la taifa, kwani itawezesha hata wafanyabiashara wadogo kulipa kodi.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Kwa Undani8 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-




Post a Comment