Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI HUKO MBEZI

Jana usiku yametokea mauwaji ya mtu mmoja mwanaume kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika Bar ya Kadabla iliyopo katikati ya Mbezi kwa Msuguli na Kibanda cha Mkaa.Mauwaji hayo yametokea kati ya majira ya saa tano usiku hadi saa saba usiku

Mashuhuda wa tukio katika eneo hilo wanasema marehemu alifika katika Bar hiyo ambayo amezoea kufika mara kwa mara anapokuwa anatoka kwenye mihangaiko yake maeneo ya K'koo,usiku wa jana alifika akiwa peke yake na kuegesha gari kisha kuanza kupoza koo.

Baada ya muda kupita,alimpigia mkewe ambaye wanaishi nae maeneo ya Mbezi Mwisho eneo la Tanesco njia ya kwenda Malamba Mawili,wito huo kwa mkewe ilikuwa kwa ajili ya kukaa wote ili waagize "kitimoto" na kuburudika pamoja.Katika ya burudani ya moja moto na mbili baridi huku kitimoto ikiwa inakaangwa jikoni kwa Mangi,walikuja watu wasiopungua wawili na kuanza kugongagonga gari lake,ilibidi aamke ili kujua kulikoni watu hao kugonga gari lake?

Baada ya maulizo hayo,wale jamaa wakamwambia wao wanataka pesa,wanajuwa ana pesa ndani ya gari,hivyo wanazitaka.Yakatokea mabishano na baadae jamaa wakampiga risasi mbele ya mke wake na kuchukua maisha yake huku wakitokomea na kiasi cha pesa kilichokuwepo.Kulizuka taharuki na watu kuacha vinywaji vyao na chakula juu ya meza na kutawanyika,hata waliokuwa "tungi" waliweza kukimbia bila kuyumba.

Msiba uko nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mbezi Mwisho(Tanesco Maghorofani) njia ya kwenda Malamba Mawili.Bwana alitoa na bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe.

Polisi iamke na kutazama matukio haya ya uhalifu maana watu wanauwa wazi wazi na silaha za moto zimeenea hovyo hovyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top