Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS ... RAIS MAGUFULI AMTUMBUA JIPU MKURUGENZI MJI BABATI


Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole. Omari Mkombole alihamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati na kupelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma mwishoni mwa mwaka jana.

Raisi aliyasema hayo leo mchana katika mji wa Babati karibu na Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Babati aliposimamishwa kusikiliza kero zao wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha.

Raisi aliyasema hayo alipoulizwa na mwananchi mmoja kero za ardhi zinazowakabili hasa zinazohusu Shamba la Makatanini. Raisi alimjibu mwananchi kwamba taarifa zote za ardhi anazo na anazishighulikia. Raisi akasema amemsimamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa tuhuma zinazohuzu uuzajia wa ovyo wa shamba la makatanini.

Kusimamishwa huku kumekuja baada ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Kocha Joel Bendera na kugundua kero nyingi na ubadhirifu katika mradi wa kuuza viwanja katika shamba la Makatanini na sekta nyingine zinazosimamiwa na Halmashauri ya Mji wa Babati.

Source: JF
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top