Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FILAMU YA "IMEBUMA" YAPIGWA STOOOOP

Bodi ya Filamu Tanzania imesitisha usambazaji wa filamu ya “Imebuma” mpaka pale maudhui yake yatakapofanyiwa marekebisho.

Akisitisha usambazaji wa filamu hiyo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso amesema mtengenezaji wa filamu hiyo hana kibali cha kutengenza filamu kutoka Bodi ya Filamu na hajazingatia Sheria na kanuni za utengenezaji wa filamu.

Bi Joyce Fisso amesema filamu hiyo imesitishwa kwenda sokoni kutokana na kukiuka vifungu vya kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 2011 ambayo inakataza kuonesha namna yoyote ya udhalilishaji wa kibinadamu katika filamu na maigizo.

“Baada ya kuangalia kwa makini filamu hii na kuona mapungufu ambayo yanakinzana na Kanuni za Sheria ya filamu na Michezo ya kuigiza  nimeamua kuisitisha usambazaji wake mpaka pale wahusika watakaporekebisha maudhi yake”Alisema Bi Joyce.

Bi Joyce amefafanua kuwa filamu hiyo imeonesha baadhi ya matukio ya udhalilishaji wa kibinadamu, ushawishi wa matendo ya ngono na ushoga ambayo ni kinyume na madili ya mtanzania.

Aidha kwa upande wake Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Julius Tairo amewataka waandaaji na waigizaji wa filamu nchini kufanya utafiti wa kutosha kuhusu maudhui ya filamu kabla ya kutengeneza ili kuondokana na  utengenezaji wa filamu zisizofata Sheria na kanuni za utengenezaji wa filamu Tanzania.
Muhusika Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda) akimbembeleza muigizaji na mtayarishaji wa filamu hiyo  Bi Sarah  Nyika (Asha Mauno) mara baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kusitizasha  usambazaji wa filamu hiyo leo. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top