Klabu ya Yanga kupitia kwa mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Jerry Muro, wamesema wako tayari kuisaidia Simba kulipa deni la Musoti ili klabu hiyo ya Msimbazi isishushwe daraja.
Muro amsema, wako tayari kuichangia Simba kulipa deni lao linalowakabili ili FIFA isiishushe daraja na wao wakakosa pointi sita katika msimu ujao wa VPL.
“Tunaomba watuletee barua na karatasi za malipo za yule mchezaji ili sisi tu-process malipo kwa sababu tuliahidi tukifika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika tutawasaidia kulipa deni lao. Sisi hatukubali Simba ishushwe daraja kwasababu pale tunapointi sita za wazi kwenye msimu ujao wa ligi”.
“Sasa kwanini tukose pointi sita ambazo tunaweza tukazitetea zikabaki. Inaweza ikashuka Simba halafu ikapanda timu ya Milambo ya Tabora halafu ikatusumbua sana, sisi tunazihitaji ponti sita za Simba na tulisema tukifika hatua ya makundin tutawalipia”.
“Ili tuweze kufanya transaction na kwakua hela hii inalipwa kupitia FIFA, tutawaandikia CAF barua ya kufanya malipo kwenda FIFA ili kuisaidia Simba isishuke daraja. Mhasibu wetu anasubiri karatasi za malipo na kwakua malipo yanafanyika kwa dollar, tutawaandikia CAF watoe kiasi cha pesa kwenda FIFA kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu”.
Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Duniani Leo
1 hour ago
Post a Comment