Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAELFU WAMUAGA PAPA WEMBA ... SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU ZA MAMOMBOLEZO


Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba.

Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast.

Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa.Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi hadi jumatano atakapozikwa.

Amepewa tuzo kwa mchango wake nchini humo.Rais Kabila awarded him one of the DR Congo’s highest honours for the “loyal and eminent services given to the nation”.

Msanii huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano.

Wengi waliitambua sauti hiyo na utunzi wake.Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.

Gwiji huyo wa muziki wa Lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba.
Yeye alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.

Alikuwa akimfuata mamake katika matanga na hivyo akaibukia kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza.
Mfalme huyo wa muziki wa Rhumba, mwenye umri wa miaka 66 aliaga dunia ghafla 24 April akiwa nchini Ivory Coast. 



Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top