Mbunge wa jimbo la Pangani Mkoani Tanga Jumaa Aweso (CCM) amewataka wabunge kutembea na chupa za spiriti ili kumsaidia Rais Dkt. John Magufuli kutumbua majipu.
Aweso ameyasema hayo katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma alipokuwa akitoa mchango wake ambapo amejikita katika kuelezea namna Rais anavyotumbua majipu na kuleta heshima kwa nchi hivyo kuwataka wabunge kuunga mkono jambo hilo.
Mbunge huyo amesisitiza kwamba lengo la kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli katika kuleta heshima serikalini ambapo Rais akitumbua na wabunge wakiweka spiriti majipu hayo yatakoma.
Aidha Mbunge huyo ameitaka serikali kutokuendeleza madeni sugu na kuwalipa wafanyakazi kwa haraka ili kuileta tanzania mpya
Loading...
Post a Comment