Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKE WA MTU ABAMBWA AKICHEPUKA GARINI

mke (2)Mwanamke huyo baada ya kunaswa na OFM
DAR ES SALAAMA: Noma sana! Mwanamke mmoja aliyedaiwa kuwa ni mke wa mtu (jina lake halikuweza kufahamika mara moja), hivi karibuni alinaswa akichepuka ndani ya gari katika kiwanja maarufu cha biashara ya ukahaba kilichopo maeneo ya Upanga jijini Dar.
Awali, chanzo chetu kinachofanya biashara ya kuuza chipsi katika eneo hilo kilimpigia simu mmoja wa waandishi wa OFM na kudai kuwa, mwanamke huyo amekuwa akifika eneo hilo kwa lengo la kujiuza na mara nyingi hufanya mapenzi na wanaume kwenye magari.
Sosi:  Haloo…hapo ni OFM?
Amani: Ndiyo, tukusaidie nini?
Sosi: Wala sihitaji msaada ila kuna stori ya mwanamke mmoja hapa maeneo ya Jolly Club, inadaiwa ni mke wa mtu na anakuja kujiuza kila siku. Kama vipi mje kumfuatilia mpate habari yake.
mke (1)Amani: Ulijuaje kuwa ni mke wa mtu?
Sosi: Wenzake wakija hapa kwangu kununua chips huwa nawasikia wakimjadili na kusema badala ya kutulia kwake anakuja kubanana nao.
Amani: Tunashukuru kwa taarifa, tutaifanyia kazi.
Baada ya kupata ‘tipu’ hiyo, makamanda wa OFM walijipanga ambapo juzikati walifika eneo hilo mishale ya saa sita usiku na kukuta wanawake kibao wakiwa kibiashara zaidi huku magari mawili yakiwa yamepaki pembeni mwa barabara.
Dakika chache baada ya OFM kufika eneo hilo wakiwa kwenye usafiri wa bodaboda, gari moja liliondoka likabaki moja ambapo ghafla alitoka mwanamke akiwa amevaa kigauni kifupi na kukimbia kwenda kujificha kwenye kiuchochoro, akaliacha gari alilokuwa amepanda likiondoka kwa spidi.
mke (3)Kufuatia mazingira hayo, paparazi wetu alifanikiwa kumpiga picha mwanamke huyo aliyekuwa akikimbilia gizani huku akijitahidi sana kuificha sura yake na wengine kutimua mbio baada ya kubaini wamevamiwa.
Biashara ya uchangudoa katika Jiji la Dar imekuwa ikishamiri kila siku licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi kuitokomeza ambapo wengi wanaoifanya hujitetea kuwa wanalazimika kutokana na ugumu wa maisha.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top