Meneja wa msanii wa Bongo fleva na mshindi wa BSS Kayumba Juma, Saidi Fella amefunguka juu ya kukata kwa mkwanja wa msanii huyo kabla ya mjengo wake kukamilika.
Akizungumza na eNewz Fella alisema kuwa mkwanja wa msanii huyo mpaka sasa umeshakatika kutokana na matumizi mengine ambayo yalikuwa ni ya muhimu hivyo atachelewa kuwaonesha mashabiki zake kama ambavyo alikuwa amewaahidi hapo awali.
“Pesa yake ilitumika kwa ajili ya kutengeneza video, kununulia gari pamoja na kuijenga nyumba yake hadi pale ilipofikia ila kwa sasa nategemea Kayumba aanze kupige shoo ili aweze kuingiza pesa itakayosaidia kumalizia kujenga nyumba yake,” alisema Fella.
Pia katika mahojiano yake ya awali na eNewz Kayumba aliwaahidi mashabiki zake kuwa atawaonesha mjengo wake anaoujenga ikiwa ni sehemu ya matumizi ya shilingi milioni 50 za ushindi wake, lakini sasa imekuja kuwa tofauti.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
Kwa Undani4 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment