Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO WA KABWE AMCHUNIA MAKONDASiku ya jana ilikua ni siku ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndg. Wilson Kabwe iliyofanyika viwanja vya Karimjee katikati ya Jiji la Dar es salaam.

Katika hali ya kutoelewa nini kinachoendelea, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alijikuta akiganda kwa sekunde kadhaa mbele ya binti wa marehemu Wilson Kabwe anayefahamika kwanjina la Anna pale alipo jaribu kumpa mkono wa pole lakini binti huyo alikataa kujibu huku akibubujikwa na machozi ya uchungu.

Habari kutoka kwa watu karibu wa familia zinasema binti huyo alifanya hivyo kutokana na machungu aliyokuwa nayo juu ya Makonda ambae wiki za usoni inaeleweka ya kwamba Mkuu huyo wa mkoa alikuwa mstari wa mbele kuchochea moto ambao ulisababisha Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo .

Habari za ndani zinasema kitendo hicho cha binti huyo cha kukataa mkono wa Makonda kimetokana na hotuba aliyotoa Mh. Makonda ambayo kwa maudhui ilikua imejaa utukufu binafsi ya kitendo alichofanya akisema "Kaka yangu kabwe ameondoka lakini huu sio mwisho wa kupambana na mafisadi".

Mpaka habari hizi zinatufikia tulijaribu kuwasiliana na msemaji wa familia lakini jitihada zetu ziligonga mwamba kwani alikua hapatikani.. Source: Tz Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top