Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO WA KIGODA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI UNEC

Mbunge wa Handeni, Omar Abdallah Kigoda 

Handeni. Mbunge wa Handeni, Omar Abdallah Kigoda ameibuka kidedea katika uchaguzi wa kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wilaya ya Handeni.

Akitangaza matokeo hayo jana, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Tanga, Methew Mganga alimtaja Kigoda kuwa mshindi kwa kupata kura 101 kati ya 180 zilizopigwa.

Kigoda anashika nafasi iliyoachwa na baba yake, Dk Abdallah Kigoda baada ya kufariki dunia. Aliwashinda wapinzani wake Maajabu Hamis, Mussa Kidato, Athuman Lukoya na Hamis Mnondwa.

Pia, Farida Mashaka alichaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa.

Akiwashukuru wanachama, Kigoda aliahidi kufanya kazi kwa bidii bila kujali itikadi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni, Athuman Malunda alisema siasa inahitaji uvumilivu na kuwataka ambao kura hazikutosha kuvunja makundi.

na badala yake wakijenge chama chao ili waweze kuisimamia serikali kwa umoja wao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top