Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

POLISI "YAMKWEPA" MAALIM SEIF

Jeshi la Polisi Zanzibar limeahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa sababu zilizoelezwa kuwa nje ya uwezo wake.

Katika barua yake kwa Maalim Seif iliyosainiwa na DCP Salum Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, haikutaja ni lini mahojiano hayo yatafanyika lakini imesema, “Tutakujulisha mapema siku ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu”.

Barua hiyo ya Mei 26 imenukuu barua ya awali ya Mei 22, 2016 iliyomuita mwanasiasa  huyo makao makuu ya polisi Zanzibar kwa mahojiano kuhusu, “masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa visiwa hivi.”

Kutokana na hatua hiyo, Maalim Seif aliyetarajiwa kuwasili jana saa 3 asubuhi Zanzibar kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa aliahirisha safari hiyo na kuwasiliSaa 10  jioni kwa ajili ya maandalizi ya ziara yake ya kichama kuanzia leokatika wilaya  saba za Unguja.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top