Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC AAGIZA MKURUGENZI NA MHAZINI KUKAMATWA

MKUU wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo ameagiza polisi mkoani humo kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon Mayeye na aliyekuwa Mweka Hazina, Emmanuel Joramu ili waweze kuhojiwa kuhusu ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za serikali.

Mulongo ametoa agizo hilo juzi kwenye kikao cha majumuhisho ya ziara yake aliyoifanya wilayani Bunda na kuagiza kuwa watuhumiwa wote wakabidhiwe kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG).

Agizo hilo alilitoa kutokana na taarifa ya baraza la madiwani iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Issack Mayela inayohusu ubadhirifu huo wa mamilioni ya fedha ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 2.3, zikiwemo za ulipaji fidia wananchi wa kijiji cha Tairo ili kupisha eneo la uwekezaji (EPZ).

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa watumishi hao wa serikali ambao kwa sasa wamehamishiwa katika halmashauri nyingine watafutwe popote pale walipo na wakamatwe mara moja na kuhojiwa na kisha kutoa maelezo yao polisi, ikiwa ni pamoja na hatua za kinidhamu na za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

“Huyo Mkurugenzi na Mweka Hazina ambao wametajwa katika taarifa hizo watafutwe mahali popote walipo na kisha kuhojiwa dhidi ya ubadhirifu huo na hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe dhidi yao…kazi hii naikabidhi CAG na Takukuru na waikamilishe ndani ya siku 14,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top