Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YAKAMATA KILO 140 YA DAWA ZA KULEVYA

Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.

Serikali imefanikiwa kukamata takribani kilo 139.69 za dawa za kulevya ikiwemo kilo 53.49 za Heroin, Cocaine kilo 86.2 kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Habari na Takwimu wa tume hiyo, Amani Msami, pia tume hiyo imekamata tani 97 za bangi na mirungi.

Alisema mbali na kukamata kilo hizo, takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa hizo kwa njia ya kujidunga sindano.

“Serikali imefanikiwa kukamata takribani kilo 53.49 Heroin, Cocaine kilo 86.2 kuanzia mwaka 2015 mpaka Aprili mwaka huu” alisema Msami na kuongeza kuwa:

“Watumiaji wa Heroin nchini wanakadiriwa kuwa kati ya 200,000 hadi 425,000 ambapo kati ya hao 30,000 hutumia dawa hiyo kwa njia ya kujidunga”.Msami alifafanua kuwa mbali na kukamata dawa hizo, tume hiyo ilikamata tani 81.3 za bangi na Mirungi tani 15.7.

Aliongeza kuwa mbali na hayo idadi ya watuhumiwa waliyokamatwa wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya zikiwemo Bangi,Mirungi, Heroin na Cocaine walikuwa 14,503.Hata hivyo, alisema takwimu hizo zinaonyesha jitihada za serikali katika kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya nchini na si ukubwa wa usafirishaji wa Heroin na Cocaine nchini.

“Moja ya jitihada za Serikali katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya ni kutungwa kwa Sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya mwaka 2015.” Alisema Msami.

Alifafanua kuwa sheria hiyo imeweka adhabu kali kwa makosa ya kujihusisha na matumizi na biashara ya dawa ya kulevya ikiwemo kifungo cha maisha kwa yeyote atakayesafirisha dawa za kulevya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top