Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SNURA AKUBALI YAISHE


Mwimbaji wa muziki wa Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya muziki unaoitwa "Chura".

Akizungumza na vyombo vya habari leo Snura amesema wakati wa utayarishaji wa video hiyo mvua ilinyesha hivyo madansa walilowana.

"Baada ya kuona wamelowa ilibidi tusitishe kupeleka katika televisheni na kuiacha you tube, Snura hajafungiwa bali video yangu ilisitishwa na mimi nilizuiwa kujihusisha na sanaa mpaka nijisajili," amesema Snura.

Meneja wa mwanamuziki huyo Hemedi Kavu amesema tayari walishakwenda Basata tangu jana kuomba usajili, leo wamepatiwa cheti cha usajili.

"Tumeshajisajili Basata, pia tayari tumeshaitoa video hiyo kwenye mtandao wa YouTube, tumeshalitekeleza na akaunti ya wimbo huo imeshafutwa na tunatarajia kuifanya video hiyo upya," amesema Hemedi Kavu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top