Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UHUSIANO WA U-GENIOUS NA UKICHAA

Kumekuwa na theory nyingi mitaani kuwa watu wenye intelligence kubwa na ma-genius wengi wana tabia nyingi za ukichaa au ni vichaa kabisa, madaktari bingwa wengi kwenye mahospitali makubwa hapa nchini ambao wanategemewa wengi huwa ni "wehu".

Hata katika viunga vya vyuo vikuu maprofessor wengi wakubwa wa kuaminika wengi huwa ukikaa nao utagundua tu wana-"wehu" fulani.

Ukifuatilia biography nyingi za watu waliokuwa na uwezo mkubwa wa kiakili na wavumbuzi wengi wakubwa hapa duniani katika sayansi na katika sanaa utagundua historia zao zimegubikwa na uchaa wa hali ya juu.

Mtu kama Isaak Newton inasemekana alikua na magonjwa ya akili na saikolojia ambayo kwa sasa kitaalamu yanaitwa "schizophrenia", huu ni ugonjwa wa mtu kutokuweza kuishi na mtu yeyote,historia inaonesha Newton alikuwa ni mtu wa kujistukia muda wote kama mtu aliyeua vile, na mara nyingi aliwashutumu ndugu zake kuwa wanataka kumuwekea sumu kwenye chakula .Alipofika miaka 40 hali ilikua mbaya zaidi na alikua hawezi kuishi hata na ndugu zake wa karibu akajitenga completely .

Albeit Einstein yeye alikua na tabia ya uchafu uliopindukia, inasemekana chumba alichokuwa akiishi kilikua kama zizi la nguruwe, kula hapo hapo kujisaidia hapo hapo hakuna mtu wakawaida anayeweza kuingia ndani, kilikua kinanuka kwa uvundo lakini pia hata nguo zake alikuwa anaweza kuvaa miezi bila kufua na kutokana na tabia yake ya uchafu na kutokujipenda na kutopenda kunyoa wengi walijua ni mwehu, wataalamu wa magonjwa ya akili kwa sasa wanauita ugonjwa huu schizotype.

Alexander Graham Bell, huyu ni mvumbuzi wa simu, yeye alikua na tatizo la hisia kali za mapenzi , hisia zilizopitiliza mpaka alikuwa kero kwa mpenzi wake miss Hello. Inasemekana alikua kama zombi kabisa kwa mpenzi wake kuna nyakati ilibidi mpenzi wake huyu amkimbie, lakini pamoja na kumkimbia huku siku alipovumbua tu simu neno la kwanza katika simu lilikua ni kutaja jina la mpenzi wake HELLO na hapo ndio utamaduni wa kuanza na neno HELLO kwenye simu ulipoanzia, japo watu wa kizazi hiki wanachukulia kama ni fashion lakini neno HELLO lilitajwa na mtu aliyekuwa na emotion breakdown wakati huo .

Martin Luther huyu alikua na tatizo la misongo ya mawazao iliyotukuka (chronical depression), lakini pia alikua ni mtu mwenye "mizuka ya ajabu, siku akiamka kichwa kimemtuma kufanya kazi anaeza fanya kazi hata 48 hrs non-stop, siku kichwa kikimtuma kusoma anaweza kusoma hata 36 hrs non-stop. Mwaka 1517 kichwa kilimtuma kuandika Thesis za kupinga namna Kanisa Katoliki linavyoendeshwa, aliandika thesis 95 alipoona hawamuelewi akaamua kuzibandika mlangoni mwa kanisa la Wittenberg halafu akasepa, na hapo ndipo ikaanza movement ya protestant churches.

Wapo wengi kama Thomas Edson, Leonardo da Vinci, Michelangelo Buonarroti, Theodore Roosevelt,John Nash,Michael Faraday, Henry Ford na wengine kibao ambao historia zao zinapatikana kiurahisi, wote hawa wameonesha kuwa na degree fulani ya ukichaa ambayo ni tofauti na mtu wa kawaida kama ambavyo sayansi ina-define na wengi wamekuwa na tabia ya kuongea wenyewe muda wote.

Kuna vitabu vimeandika research ya hii kitu na wakafanya clinical trials wakagundua kuwa asilimia kubwa za watu wenye akili nyingi au ma-genius familia zao pia kuna vichaa wengi au watu wenye upungufu wa akili au wehu.

Moja ya kitabu kizuri ni cha mwanamama Nancy C. Andreasen, M.D., Ph.D. kinaitwa "The Creating BRAIN, Neurosciences of Geinus" kimejaribu sana kutafiti kwa kutumia technolojia nzuri ya MRI bongo nyingi za ma-genius na kimegundua zinafanana neuro-arrangement zake na kua sehemu za brain zao haziko developed kabisa.

Swali hapa linakuja je kuna uhusiano gani kati ya kuwa na Intelligence kubwa au kuwa genius au kuwa highly creative na UKICHAA??
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top