Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAFANYAKAZI WA NDANI HAWAKAMATIKI

Dar es Salaam. Licha ya baadhi  yao kudaiwa  kuvunja ndoa, kuiba na kunyanyasa watoto, kwa sasa wafanyakazi wa ndani wanatafutwa kama lulu.

Mahitaji ya wafanyakazi hao,  maarufu kwa jina la house girl  au ‘dada wa kazi’, unatokana na ukweli kuwa mchango wao  kwenye familia za kisasa unazidi kuwa mkubwa, huku idadi ikizidi kupungua, Mwananchi imebaini.

Wafanyakazi wa ndani wanatumia muda mwingi pamoja na watoto kuliko wazazi, wanawezesha wanawake wenzao kushiriki kikamilifu kutumia fani zao makazini na wakati mwingine kwa watoto wa mzazi mmoja, wafanyakazi hawa wanatoa faraja kwa mzazi katika kushirikiana kulea.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa wafanyakazi wa ndani wanatafutwa kwa udi na uvumba, hali ambayo pia imeongeza idadi ya mawakala  wanaotafuta wasichana vijijini na kuwaleta mijini na baadhi ya nchi  kwa ajili ya kufanya kazi hizo.

 Kadhalika, imebainika kuwa kwa sasa wafanyakazi hao wa ndani wamekuwa wakitumiwa na mawakala hao kufanya kazi eneo moja  kwa muda mfupi, kisha kuondoka au kutoroka  na kwenda sehemu nyingine kufanya kazi kwa mishahara mikubwa zaidi.

Hali hiyo inatajwa kuwa inasababisha familia kubadili wafanyakazi wa ndani kuanzia watano hadi kumi kwa mwaka kutokana na wengi kuibua sababu tofauti na kuondoka baada ya kukaa muda mfupi kwa mwajiri mmoja.

Kutokana na kuwa  nadra  kwa sasa, Mwananchi ilibaini kuwa akinamama wamefikia hatua ya  kuiba mfanyakazi wa ndani kutoka kwenye familia moja kwenda nyingine.

Kadhia hii ya wasichana wa kazi inawakumba zaidi wanawake walioajiriwa au wanaofanya biashara na wenye watoto wadogo ambao huhitaji mtu wa kuangalia nyumba wakati wasipokuwapo.

Hata hivyo, wengi waliowahi kuajiri wasichana wa kazi wana malalamiko lukuki, hasa wizi, watoto kunyanyaswa, ushirikina na kutembea na watoto wa mwenye nyumba au baba.

Mwanamke mmoja mkazi wa Njombe, Flora Mwenegoha alisema alipata msichana wa kazi ambaye alikiri kuwa babu yake ni mchawi.

“Siku moja alipandisha mashetani, akisema ana jini  mahaba, ametumwa aje kuvunja ndoa kwenye nyumba hiyo,” alisema Mwenegoha

 Mwenegoha, aliyekuwa na ujauzito wakati huo, hakuwa na la kufanya zaidi ya kumuondoa binti huyo. Alipata yaya mwingine ambaye naye alifanya kazi kwa miezi minne kabla ya kuondoka, akidai anataka kuolewa.

“Tangu nina mimba ya miezi saba na sasa mtoto ana mwaka mmoja, nimebadili ma ‘house girl’ wanne. Hili si janga hili jamani,” alisema.

‘House Girl alivunja ndoa yangu’

Pamoja na kuwa adimu, wasichana hao wameivunja ndoa ya Maia Yusufali, raia wa Tanzania mwenye asili ya Dubai.

 Yusufali alisema dada wa kazi aitwaye Kuluthum Hussein alitembea na mumewe kwa muda wa mwaka mmoja bila yeye kujua.

 “Nilipokuja kujua, nikahamaki na nikagombana na mume wangu, cha ajabu mume akaniambia nichague aondoke Kuluthum au mimi. Nikaamua kuondoka. Hivi ninavyokuambia kamuoa Kuluthum na amezaa watoto naye,” alisema.

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Tausi  Mbowe alisema alipata msichana wa kazi ambaye alikuwa mlozi, na kueleza kuwa ilikuwa vigumu kumtambua, lakini siku moja alipika chakula na kukataa kukila.

Alisema baada ya familia kula chakula walikumbwa na ugonjwa wa  kuhara kwa wakati mmoja, walipomuuliza msichana huyo alikana kuhusika kwa lolote.

“Siku moja tulimtembelea mama yangu, kufika huko akakataa kula chakula. Mama alimbana lazima ale akaanza kupandisha mapepo akawa anajikaba. Alipobanwa akasema bibi yake humchukua na kwenda kula nyama za watu usiku. Tulistaajabu,” anasimulia.

Alisema hata waliporudi nyumbani hali ilikuwa ile ile na maneno yaleyale na ndipo walipoamua kumuondoa.

Hata hivyo, anabainisha kuwa wapo ambao wanatumwa kutoka majumbani mwao kuvunja ndoa za watu kwa kumtega mwenye nyumba.

Alisema miaka kadhaa iliyopita alipata tatizo la mtoto kunywa mafuta ya taa, ambalo lilitokana na msichana wa kazi kuondoka nyumbani na kumwacha mtoto peke yake.

“Nilipigiwa simu mtoto wangu amekunywa mafuta ya taa, nilipofika hospitali nikakuta mtoto hali yake mbaya kumbe dada aliondoka na kumwacha peke yake ameenda kwenye mambo yake nyumba ya jirani, mtoto  kuona chupa yenye maji akanywa kumbe ni mafuta ya taa, dada aliondoka mchana akarudi jioni,” alisema Tausi.

Aliongeza kuwa wasichana wa kazi wengi alioishi nao wamekuwa na tabia ya kuanzisha uhusiano wa mapenzi na madereva bodaboda, wauzaji wa maduka na magenge.Mawakala

Uchunguzi wa mwananchi umebaini kuwapo kwa mawakala  wanaouza wasichana wa kazi jijini Dar es Salaam, ambao pia wakifika kwenye nyumba za mabosi wao hukaa siku chache kisha kuondoka.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top