Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATENDAJI WATAFUNA BIL 1.4 ZA UCHAGUZI

MKUU wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Senyi Ngaga amewajia juu baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo waliohusika kufanya ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.

Fedha hizo zilitolewa na serikali kwenda wilayani humo, kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kufanya kazi iliyolengwa katika uchaguzi mkuu.

Alisema ubadhirifu huo umebainika baada ya ofisi yake kuunda tume ndogo iliyofanya kazi kwa ushirikiano wa baraza la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo.

Aidha, alisema tume iliyoundwa ambayo inaendelea na uchunguzi wake, taarifa za awali katika fedha hizo zinathibitisha maofisa waliopewa dhamana ya kuendesha uchaguzi huo wilayani hapa kwa kushirikiana na idara ya fedha ya wilaya ya Mbinga, ndio wanaodaiwa kuhusika kutengeneza mianya ya kutafuna fedha hizo.

Hayo yalisemwa na Ngaga kwenye kikao cha baraza la Madiwani jana kwenye ukumbi wa Umati mjini hapa na kwamba ubadhirifu huo umefanyika kupitia watu kulipana posho, ununuaji wa mafuta na vipuri vya magari, chakula na vifaa vingine vya ofisi, kinyume na taratibu za miongozo iliyotolewa na serikali.

Alifafanua mpaka sasa kati ya fedha hizo zilizotolewa na NEC wamebaini ubadhirifu wa Sh milioni 513 ambazo hazikufuata taratibu na miongozo husika katika matumizi yake.

Kati ya hizo Sh milioni 822 zimetumika watu kulipana posho, Sh milioni 140 kwa ajili ya kusambaza vifaa vya maofisini, Sh milioni 135 zimetumika kununua vipuri vya magari na mafuta na kwamba Sh milioni 85 zimetumika kwa ajili ya chakula.

Akitolea mfano juu ya fedha zilizotumika kununulia vifaa vya ofisi Sh milioni 140, alisema kuwa tume hiyo aliyoiunda kuchunguza matumizi ya fedha hizo imebaini kuwa fedha zilizotumika kununulia vifaa hivyo ni Sh milioni nne tu na sio zaidi ya fedha hizo, ambapo suala hilo lilithibitishwa baada ya tume kumhoji mzabuni husika ambaye alipewa kazi ya kusambaza vifaa hivyo vya ofisini.

Pia alieleza kuwa fedha zilizotumika kununulia vipuri vya magari Sh milioni 135 mzabuni aliyetumika kufanya kazi hiyo, hana duka au kampuni ambayo ingeweza kumfanya aweze kuwa na sifa katika mchakato wa manunuzi ya vifaa husika jambo linaloleta mashaka na kujenga mianya ya wizi wa fedha za umma.

Aliongeza kuwa ameshangazwa na ofisi ya Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Mbinga kutofanyia kazi ipasavyo na kutolea taarifa katika vikao vya baraza la madiwani huku akiagiza na kumtaka mkaguzi huyo kuhakikisha kuanzia sasa anafanya kazi zake kwa uwazi.

Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Ambrose Mtarazaki amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Samwel Komba kuhakikisha anafanya kazi kwa karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya ili wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi ili iweze kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top